Huenda Duterte asikubali mwaliko wa Trump

Trump alimpa mwaliko Duterte wakati wa mazungumzo kwa njia ya simu kati ya wawili hao siku ya Jumamosi Haki miliki ya picha EPA
Image caption Trump alimpa mwaliko Duterte wakati wa mazungumzo kwa njia ya simu kati ya wawili hao siku ya Jumamosi

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amesema kuwa huenda asikubali mwaliko wa Rais Donald Trump nchini Marekani.

Rais Duterte alisema kuwa hawezi kutoa ahadi yoyote ya kusafiri kuenda Marekani kutokana na shughuli nyingi na safari anazopanga kufanya nchini Urusi na Israel.

Bwana Trump alimpa mwaliko Duterte wakati wa mazungumzo kwa njia ya simu kati ya wawili hao siku ya Jumamosi

Rais huyo wa Ufilipo alikuwa amesrma kuwa yuko tayari kuboresha uhusiano na Marekani.

Alisema kuwa tofauti zake na Marekani zilikuwa wakati wa kipindi cha Rais Barack Obama ambaye wakati mmoja alimuita kuwa mtoto wa kahaba.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ziara hiyo itakuwa fursa ya kujadili umuhimu wa ushirikiano kati ya Marekani na Ufilipino

Wakati wa mawasiliano viongozi hao wawilia walizungumzia vita vyenye utata dhidi ya madawa ya kulevya vinavyoongozwa na Rais Duterte ambavyo vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 7000 chini ya mwaka mmoja.

Suala la Korea Kaskazini nalo liliibuka.

Ziara hiyo itakuwa fursa ya kujadili umuhimu wa ushirikiano kati ya Marekani na Ufilipino ambao kwa sasa unakua mzuri.

Mkutano kati ya Bwana Duterte na Obama ulifutwa baada ya Durtete kumtukana Obama.

Maelfu ya walanguzi wa madawa ya kulevya wameuawa na polisi huku wengi wakikamatwa.