Watoto wanaokabiliwa na utapia mlo waongezeka Somalia

Watoto wanaokabiliwa na uapia mlo nchini Somalia Haki miliki ya picha Unicef
Image caption Watoto wanaokabiliwa na uapia mlo nchini Somalia

Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia watoto Unicef limesema kuwa makadirio ya watoto wanaougua utapia mlo nchini Somalia mwaka huu yamepanda kwa asilimia 50.

Linasema kwamba takriban watoto milioni 1.4 wamewekwa katika katika orodha hiyo.

Unicef inasema kuwa watoto wanaokabiliwa na utapia mlo wanaweza kufariki mara tisa zaidi kutokana na magonjwa mabaya kama vile kipindupindu, kuharisha na ukambi ambayo yanaenea.

Somalia inakabiliwa na athari za baadaye za ukame.

Umoja wa Mataifa unasema kuwa dunia inakabiliwa na mgogoro wa kibinaadmu tangu mwisho wa vita vya dunia vya pili.

Ukame tayari umetangazwa katika maeneo kadha ya Sudan Kusini.

Pia kumekuwa na onyo la kutokea kwa ukame kaskazini mashariki mwa Nigeria Somalia na Yemen.

UN inasema kuwa takriban watu milioni 20 wanakabiliwa na baa la njaa.