Kiongozi wa kundi la mihadarati Mexico akamatwa

Damaso Lopez amekuwa miongoni mwa viongozi wa Saniola tokea kukamatwa kwa Guzman
Image caption Damaso Lopez amekuwa miongoni mwa viongozi wa Saniola tokea kukamatwa kwa Guzman

Mamlaka nchini Mexico imesema kuwa imefanikiwa kumtia nguvuni mmoja wa wanachama wa Saniola kundi ambalo awali lilikuwa likiongozwa na mfanya biashara maarufu wa dawa za kulevya Joaquin Guzman akijulikana zaidi kama ''el Chapo''.

Damaso Lopez alikamatwa katika mji wa Mexico City kwa tuhuma za kusafirisha tani za dawa za kulevya kwenda Marekani.

Image caption Guzman alikua kiongozi wa kundi la Saniola kabla ya kukamatwa

Tokea kukamatwa kwa aliyekuwa kiongozi wao Joaquin Guzman, viongozi wa juu wa Saniola wamekuwa wakihitilafiana kwa kung'ang'ania madaraka hali iliyopelekea kuibuka kwa uhalifu katika maeneo ya Saniola.