Polisi waliowauwa watu weusi Marekani kutoshtakiwa

Eneo la kumbukumbu la watu weusi waliouawa ncini Marekani kwa kupigwa risasi na polisi wazungu bila hatia Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Eneo la kumbukumbu la watu weusi waliouawa ncini Marekani kwa kupigwa risasi na polisi wazungu bila hatia

Idara ya sheria Marekani inaarifiwa kuamua kutowashtaki maafisa wawili wa polisi waliompiga risasi na kumuua mwanamume mweusi huko Louisiana mwaka jana.

Kanda ya video inaonekana kuwaonyesha maafisa hao wazungu wakimzuia chini Alton Sterling walipofyatua risasi, hatua iliozua maandamano ya siku kadhaa huko Baton Rouge.

Misa ya kumbukumbu inafanyika katika eneo alipouawa.

Afisa mwingine wa polisi mzungu nchini Marekani aliyepigwa picha akimpiga risasi mgongoni mwanamume mweusi ambaye hakujihami miaka miwili iliyopita amekiri makosa ya ukiukaji wa haki za raia.

Huenda afisa Michael Slager akahukumiwa maisha gerezani kwa kumuua Walter Scott.