Mauzo ya simu za Apple yashuka

Mauzo ya simu za Apple yadaiwa kushuka Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mauzo ya simu za Apple yadaiwa kushuka

Kampuni ya Apple iliuza simu chache ikilinganishwa na mwaka moja uliopita katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza mwaka 2017,kulingana na ripoti ya kampuni hiyo.

Kampuni hiyo kutoka jimbo la California ambayo inakaribia kuzindua simu mpya mwaka huu imesema kuwa iliuza simu milioni 50.8 katika kipindi hicho ikiwa ni upungufu wa asilimia moja.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo Tim Cook alilaumu hatua ya wateja kusubiri simu mpya ya kampuni hiyo mwaka huu.

Hisa katika kampuni hiyo zilianguka kwa asilimia 2 baada ya mauzo muda mfupi baada ya kuimarika.

Apple iliripoti kuongezeka kwa mapato hadi asilimia 4.6 ambayo ni dola bilioni 52 ikiwa ni chini na ilivyotarajiwa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Simu aina ya Apple

Kushuka kwa mauzo ya simu hizo hatahivyo kulifidiwa na huduma ikiwemo ile ya malipo ya Apple Pay, iCloud na App Store ambayo ilirekodi ongezeko la mauzo ya asilimia 18 ambayo ni dola bilioni 7.

Bwana Cook pia alizungumzia kuhusu ukuwaji wa mauzo ya saa za Apple pamoja na Airpods mbali na chombo cha kusikilizia sauti cha masikioni aina ya Beat.

Licha ya kushuka kwa mauzo, mapato ya kampuni hiyo bado yameongezeka hadi asilimia moja na kufikia dola bilioni 33.2 kutokana na mauzo mengi ya simu kubwa ya iPhone 7 plus.

Mada zinazohusiana