Waandishi wa habari wagoma kupinga kupunguzwa ajira Australia

Siku ya Jumatano Fairfax ilisema kuwa itaawachisha kazi wafanyakazi 125 Haki miliki ya picha EPA
Image caption Siku ya Jumatano Fairfax ilisema kuwa itaawachisha kazi wafanyakazi 125

Waandishi wa habari katika shirika la habari la Fairfax Media, moja ya wachapishaji wakubwa zaidi nchini Australia wamefanya mgomo kwa wiki moja wakilalamikia kupunguzwa kwa nafasi za ajira.

Siku ya Jumatano Fairfax ilisema kuwa itaawachisha kazi wafanyakazi 125 ambayo ni robo ya wafanyakazi wa chumba cha habari.

Kujibu hilo sasa wafanyakazi watagoma hadi baada kusomwa kwa bajeti wiki ijayo ambayo ni siku kubwa kwa vyombo vya habari.

Sawa na mashirika mengine ya habari kote dunaini, Fairfax inakumbwa na changamoto za kushuka kwa mauzo ya magazeti yake na kupungua na pesa zinazotokana na matangazo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Matawi ya Fairfax's ni pamoja na Sydney Morning Herald, The Age la mjini Melbourne na Australian Financial Review

Matawi ya Fairfax's ni pamoja na Sydney Morning Herald, The Age la mjini Melbourne na Australian Financial Review

Tangazo hilo la kupunguza wafanyakazi limetangazwa sawa na mipango ya kuanza kutumia waandishi wa habari wa kujitegemea.

Muungano wa vyombo vya habari nchini Australia ambao unawaakilisha waandishi wa habari nchini humo, umekosoa vikali mipango hiyo ya kupunguza wafanyakazi kama hatua mbaya.

Fairfax ndiye mshindani mkubwa wa shirika la Rupert Murdoch la News Corp Australia, amablo nalo linakumbwa na matatizo ya kifedha na ambalo limetangaza kupunguza wafanyakazi.