Msanii wa Playboy akosolewa kwa kupigwa picha za utupu akiwa juu ya mlima

Jaylene Cook akiwa juu ya mlima Taranaki Haki miliki ya picha INSTAGRAM
Image caption Jaylene Cook akiwa juu ya mlima Taranaki

Kwa watu wengi ambao wana tamaa ya kupata picha ya kuweka kwenye mitandao ya Facebook na Instagram, kufika kilele cha mlima na kuangalia mawingu chini yaka, unawez kuwa wakati muafaka wa kupigwa picha.

Na kama wewe ni masaniiwa jarida la Playboy, menye mashabiki 300,000, mbona usifua nguo zako na haraka kupigwa picha.

Hili ndilo lililotokea wakati Jaylene Cook alikwea mlima wa Taranaki nchini New Zealand.

Hata hivyo jamii ya Maori ya eneo hilo inasema kwa hatua hiyo inaenda kinyume na tamaduni.

Kilele cha mlima huo ni eneo takativu kwa jamii ya Maori.

Haki miliki ya picha Huw Evans picture agency
Image caption Mlima Taranaki uko magharibi pwani mwa New Zealand

"Ni kwa mfano mtu kuenda katika makao ya Vatican na kupiga picha ya utupu." msemaji wa jamii ya maori alisema.

"Ni eneo takatifu na kitu kama hiki sio kizuri."

Picha ya Bi Cook, ambaye mwenyewe ni kutoka nchini New Zealad, ilichukuliwa wakati alikwea mlima huo siku chache zilizopita.

Baada ya kuchapishwa katika mtandao wake wa Instagram akiwa umbalia wa mita 2,518 kileleni mwa mlia picha hiyo imepata karibu mashabiki 10,000.

Kwa jamii ya Maori mlima huo unatambuliwa kama kabaru la wazee wa jadi.