Watu 21 wafariki katika ajali ya mgodi Iran

Mlipuko huo umetokea wakati wachimbaji wakibadilishana muda kuingia na kutoka
Image caption Mlipuko huo umetokea wakati wachimbaji wakibadilishana muda kuingia na kutoka

Waokoaji nchini Iran wameopoa miili ya watu 21 baada ya kutokea mlipuko mkubwa katika mgodi mmoja wa makaa ya mawe, huku zaidi ya wengine 69 wakijeruhiwa.

Mlipuko huo unadhaniwa kusababishwa na kuvuja kwa gesi katika mgodi wa Zemestan-Yurt Kaskazini mwa jimbo la Golestan.

Image caption Waokoaji wakijaribu kupunguza kiwango cha gesi ndani ya mgodi

Baadhi ya miili hiyo ni ya watu waliokwenda katika mgodi huo kuwasaidia waliojeruhiwa.

Zaidi ya wachimbaji wengine 32 wamekwama ardhini.

Image caption Magari ya huduma ya kwanza yakisubiri majeruhi kuwapeleka hospitalini

Juhudi za uokoaji zinaendelea huku zikikwamishwa na njia nyembamba ya kuingia sambamba na uwepo wa kiwango kikubwa cha gesi ndani ya mgodi huo.