Waandamanaji zaidi wameuwawa Venezuela

Image caption Baadhi ya waandamanaji,Venezuela

Idadi ya vifo katika kipindi cha mwezi mmoja nchini Venezuela imeongezeka na kufikia zaidi ya watu 30, idadi hiyo imeongezeka baada ya waandamanaji kupambana tena na polisi wa kuzuia ghasia siku ya jumatano.

Kumekuwa na Ripoti kuwa watu wengi wamejeruhiwa, baadhi yao wamejeruhiwa na mabomu ya petroli yaliyokuwa yanarushwa na vijana waliofunika nyuso zao mjini Caracas waliokuwa wakiandamana kuelekea kwenye eneo la Bunge la kitaifa.

Image caption Mapigano dhidi ya Polisi na waandamanaji

Huku Polisi walijibu mapigo hayo kwa kuwatawanya kwa mabomu ya kutoa machozi na risasi za mpira.

Hata hivyo Rais wa nchi hiyo Nicolas Maduro ameukosoa upinzani na kusema kuwa anapambana kuilinda nchi dhidi ya ugaidi na kuwaambia wanaomuunga mkono kuwa ni juu yao kuamua mustakabali wa Nchi

Maduro amesema raia wa Venezuela wanapaswa kuchagua njia iwe ya vita au amani, kama wanataka vizuizi barabarani au wanataka uwakilishi kwenye Bunge