Bunge kufutilia mbali huduma ya Obamacare Marekani

Bunge la Marekani, wabunge wa Republican sasa wana mpango wa kufutilia mbali huduma ya afya ya Obamacare
Image caption Bunge la Marekani, wabunge wa Republican sasa wana mpango wa kufutilia mbali huduma ya afya ya Obamacare

Bunge la wawakilishi Marekani limepanga kura leo kufutilia mbali sheria ya huduma ya afya ya nafuu unaojulikana kama Obamacare.

Wanachama wa Republican wana imani kwamba sasa wana kura za kutosha.

Kevin McCarthy, kiongozi wa wengi bungeni amesema kwamba hatua muhimu imepigwa kuelekea kuidhinishwa mojawapo ya ahadi alizotoa rais Donald Trump wakati wa kampeni.

Kipengee kilichokarabatiwa kinachoahidi dola bilioni 8 kusaidia watu walio na magonjwa ya kitambo, kinaonekana kuwaridhisha waliokuwa na shaka.

Jitihada ya awali kufutilia mbali sheria hiyo mnamo Machi haikufaulu na ilikuwa mojawapo ya wakati mgumu wa siku mia moja za kwanza za rais Trump katika utawala.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii