Syria yaunga mkono pendekezo la maeneo salama

Mapigano yanaondelea nchini Syria, serikali ya taifa hilo inaunga mkono pendekezo la Urusi kuunda maeneo manne salama
Image caption Mapigano yanaondelea nchini Syria, serikali ya taifa hilo inaunga mkono pendekezo la Urusi kuunda maeneo manne salama

Vyombo vya habari nchni Syria vinaripoti kuwa serikali Damascus inaunga mkono pendekezo la Urusi kuunda maeneo manne salama yanayonuia kupunguza mapigano katika vita vya kiraia nchini humo.

Mpango huo unatarajiwa kujadiliwa katika mazungumzo ya amani katika mji mkuu wa Kazakh hii leo.

Ni jambo lililowasilishwa na rais Putin na kiongozi wa Marekani na Uturuki.

Katika siku ya kwanza ya ufunguzi wa mazungumzo hayo huko Astana, upinzani uliojihami Syria umekataa kuhudhuria mazungumzo hayo ukiitaka serikali isitishe kuyalipua maeneo yanayodhibitiwa na upinzani.