Mwanajeshi ajipiga picha akiuawa Afghanistan

Picha iliopigwa na mwanajeshi huyo wakati alipokuwa akifanya zoezi la kijeshi nchini Afghanistan
Image caption Picha iliopigwa na mwanajeshi huyo wakati alipokuwa akifanya zoezi la kijeshi nchini Afghanistan

Picha moja iliochukuliwa na mpiga picha wa jeshi nchini Marekani wakati yeye na wanajeshi wengine wanne waliuawa katika mlipuko imetolewa na jeshi la Marekani.

Mwanajeshi Hilda Clayton mwenye umri wa miaka 22 na wanajeshi wanne wa Afghanistan waliuawa wakati bomu lilipolipuka wakati wa zoezi la kijeshi mnamo tarehe 2 mwezi Juali 2013.

Image caption Picha hii ilichukuliwa na mwanajeshi mwengine ambaye alikuwa akijifunza na Clayton

Jeshi la Marekani pia lilitoa picha ya mwanajeshi wa kike wa Afghanistan ambaye mtaalam Clayton alikuwa akijifunza naye kupiga picha .

Pia alifariki.

Kifo cha Clayton ni ishara kwamba wanajeshi wa kike wanazidi kukabiliwa na hatari wakati wa mafunzo pamoja na vita na wenzao wa kiume.

Haki miliki ya picha Army
Image caption Clayton alikuwa mkaazi wa jimbo la Georgia nchini Marekani

Ajali hiyo ilitokea katika mkoa wa mashariki wa Laghman.

Jarida la jeshi lilichapisha picha hizo.

Haki miliki ya picha DVDS
Image caption Mwanajeshi katika shindano la Hilda Clayton kuwania mpiga picha bora