Nembo ya Miraa yakataliwa na msajili wa vyama Kenya

Mfanyibiashara wa Miraa nchini Kenya: Nembo ya Miraa yakataliwa na msajili wa vyama Kenya
Image caption Mfanyibiashara wa Miraa nchini Kenya

Kundi moja la wanaharakati limeikosoa afisi ya msajili wa vyama nchini Kenya kwa kukataa kutumia nembo ya miraa miongoni mwa wagombea wanaowania uchaguzi nchini humo.

Msemaji wa muungano wa wafanyikazi wa Miraa Nyamita Kimathi Munjuru alisema kuwa msajili wa vyama bado anaichukulia miraa kuwa dawa ya kulevya licha ya kuhalalishwa kisheria.

Wagombea wa kibinfasi wanahitajika kuwasilisha nembo watakazotumia katika chama hicho katika afisi ya usajili wa vyama na tume ya uchaguzi ili kuruhusiwa kugombea nyadhfa hizo.

Akizungumza na gazei la Nation nchini humo, Bwana Munjuri alisema kuwa wagombea kadhaa kutoka maeneo ya Meru, Nairobi, Mombasa,

Kisumu ,Lodwar, Garissa na Wajir waliwasilisha nembo ya mti wa Miraa ambazo ziikataliwa.

Katika barua ya malalamishi waliotuma kwa msajili huyo wa vyama na tume ya uchaguzi, Nyamita alisema kuwa wagombea huru wanazuiliwa kwa kutumia picha za mmea wa Miraa.

''Sababu pekee ya nembo kukataliwa ni iwapo imetumika na chama chengine ama mgombea mwengine'.

''Tunashindwa kuelewa kwa nini nembo ya Miraa inakataliwa na tunataka ushauri wako kuhusiana na swala hilo...Tunasisitiza kuwa Miraa ni mmea kulingana na sheria zetu'',alisema Munjuri.

Amesema kuwa msajili huyo hajajibu malalamishi yao.

''Wagombea wanapaswa kuruhusiwa kutumia nembo ya mti wa miraa wanapodhani kwamba utawasilisha maslahi ya mpiga kura'', alisema.

Kulingana na gazeti la Nation Mgombea mmoja anayegombea wadhfa wa Wadi au MCA katika kaunti ya Meru nchini humo na ambaye hakutaka kutajwa alisema aliwasilisha furushi la miraa kama nembo lakini ikakataliwa.

''Afisa mmoja katika afisi ya msajili wa vyama aliniambia kwamba miraa ni dawa ya kulevya. Nililazimika kutumia herufu za kwanza za majina yangu na sasa nitamaliza na afisa leo Alhamisi'', alisema.