Wanamuziki matajiri nchini Uingereza

Mwanamuziki wa muziki wa Pop nchini Uingereza ameongeza utajiri wake Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mwanamuziki wa muziki wa Pop nchini Uingereza ameongeza utajiri wake

Ziara ya ulimwengu na mauzo ya baadhi ya albamu yalimpatia msanii Adele kitita cha pauni milioni 40 mwaka uliopita, kulingana na orodha ya wanamuziki tajiri ya gazeti la Sunday Times.

Mwanamuziki huyo wa muziki wa Pop aliongeza utajiri wake kutoka pauni milioni 85 hadi pauni milioni 125 ikimaanisha ndiye mwanamuziki tajiri zaidi wa kike katika gazeti hilo linaloangaiza utajiri wa wanamuziki kila mwaka.

Hatahivyo ameshikilia nafasi ya 19 pamoja na mwanamuziki mwengine wa kiume katika oroadha ya wanamuziki matajiri nchini Uingereza ambayo imetawaliwa na wanamuziki wa kiume.

Paul Mc Cartney anaongoza orodha hiyo akiwa na pauni milioni 780 pamoja na mkewe.

Wanafuatwa na West End Mogul Lord Lioyd Webber, U2, Sir Elton John, Sir Mick Jagger na mpiga bendi mwenza wa Rolling stones Keith Richards.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Paul Mc Cartney anaongoza orodha hiyo akiwa na pauni milioni 780 pamoja na mkewe.

Adele anashikilia nafasi ya 19 akiwa na pauni milioni 125 pamoja na mpiga gita wa Queen Brian May.

Kuongezeka kwa utajiri wake kunadaiwa kutokana na ziara 122 za ulimwenguni ambazo zilimpatia kitita cha pauni milioni 138 mbali na ufanisi wake wa albamu yake ya tatu 25 ambayo iliuza kopi 2.4 duniani 2016.

Msanii huyo atahudhuria halfa ya muziki iliouza katika uwanja wa Wembley lakini ametoa ishara kwamba hatofanya ziara nyngine, hatua ambayo huenda ikamzuia kutajirika zaidi.

Wanamuziki tajiri Uingereza [Duru: Sunday Times)
1. Sir Paul McCartney and Nancy Shevell £780m Up £20m
2. Lord Lloyd-Webber £740m Up £25m
3. U2 £548m Up £48m
4. Sir Elton John £290m Up £10m
5. Sir Mick Jagger £250m Up £15m
6. Keith Richards £235m Up £15m
7. Olivia and Dhani Harrison £210m Down £10m
8= Michael Flatley £200m Up £2m
8= Ringo Starr £200m No change
10. Sting £185m No change
11= Eric Clapton £170m Up £10m
11= Sir Rod Stewart £170m Up £10m
13. Roger Waters £165m Up £5m
14. Sir Tom Jones £160m Up £5m
15. Sir Tim Rice £152m Up £2m
16. Robbie Williams £150m Up £5m
17. Ozzy and Sharon Osbourne £140m Up £5m
18. Charlie Watts £130m Up £10m
19= Adele £125m Up £40m
19= Brian May £125m Up £5m