Mugabe: Zimbabwe ni ya pili kwa maendeleo Afrika

Rais Mugabe anasema kuwa Zimbabwe ni taifa la pili kwa maendeleo barani Afrika Haki miliki ya picha AFP/getty
Image caption Rais Mugabe anasema kuwa Zimbabwe ni taifa la pili kwa maendeleo barani Afrika

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amesema kuwa Zimbabwe ni taifa lililoendelea zaidi barani Afrika baada ya Afrika kusini.

Amekana madai kwamba taifa hilo ni tete .

''Tuna takriban vyuo vikuu 14 na asilimia 90 ya watu wamekwenda shule ikiwa ni kiwango kikubwa zaidi barani Afrika huku akiongezea kwamba uchumi unaimarika.

Zimbabwe imekuwa ikishindwa kuwalipa wafanyikazi wa serikali na imewekwa katika nafasi ya 24 na shirika la umoja wa mataifa UNDP kwa maendeleo barani Afrika.