Upinzani Msumbiji wasema ‘vita vinakaribia mwisho wake’

Afonso Dhlakama alirejea mafichoni mwaka 2014 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Afonso Dhlakama alirejea mafichoni mwaka 2014

Chama cha upinzani nchini Msumbiji kimetangaza kwamba kimeongeza mkataba wa kusitisha vita kwa muda usiojulikana, shirika la haabri la AFP limeripoti.

Kiongozi wa chama hichi Afonso Dhlakama alizungumza na wanahabari akiwa mafichoni maeneo ya kati nchini humo.

AFP wamemnukuu akisema "huu sio mwisho wa vita, lakini ni mwanzo wa mwisho wa vita".

"Hizi ni habari njema sana kwa watu wa mzumbiji," aliongeza.

Renamo na chama tawala cha Frelimo walipigana vita vya wenyewe kwa wenyewe kuanzia wakati wa uhuru mwaka 1976 hadi mwaka 1992 mkataba wa kusitisha mapigano ulipotiwa saini.

Renamo baada ya hapo walishiriki uchaguzi mkuu wa vyama vingi vya siasa.

Lakini mzozo ulianza tena 2013 na mapigano yamekuwa yakichipuka mara kwa mara tangu wakati huo.

Mwaka 2014, vyama vyote viwili vilitia saini mkataba wa Amani lakini Renamo walianzisha tena mzozo baada ya kukataa kukubali matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2014.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii