Darlan Rukih: Nilibaguliwa kwa kuwa na jinsia mbili

Darlan Rukih: Nilibaguliwa kwa kuwa na jinsia mbili

Mkenya Darlan Rukih, 42, alizaliwa akiwa huntha, akiwa na viungo vya jinsia zote mbili kwa pamoja.

Akiwa na umri mdogo, alidhalilishwa na kubaguliwa, na kumfanya karibu akate tamaa maishani.

"Hii ilikuwa shida kati yangu na watoto wenzangu kwa sababu hawakuwa wananiona kama nafanana nao. Walijaribu sana kunitenga. Nikienda kwa wasichana wananifukuza niende kwa waume, nikienda kwa wanaume wananifukuza niende kwa wasichana."

Lakini alisaidiwa na mamake na sasa anapaza sauti yake kuwatetea huntha wenzake.