Trump kufanya ziara yake ya kwanza nje ya Marekani tangu awe rais

Rais Mteule wa Marekani Haki miliki ya picha AP

Rais wa Marekani Donald Trump atafanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi hiyo tangu awe rais baadaye mwezi huu.

Kwenye ziara hiyo yake, Bw Trump atazuru Israel, Italia na Saudi Arabia.

Aidha atazuru Vatican pamoja na makao makuu ya shirika la kujihami la mataifa ya Magharibi, NATO mjini Brussels.

RaisTrump atakamilisha ziara yake kwa kuhudhuria mkutano wa viongozi wa nchi saba kuu zilizostawi (G7).

Mkutano huo utaandaliwa Sicily tarehe 26 Mei.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii