Jaji aliyetoa matamshi ya kibaguzi ajiuzulu Afrika Kusini

Mabel Jansen alifanyiwa pia uchunguzi na jopo la majaji
Image caption Mabel Jansen alifanyiwa pia uchunguzi na jopo la majaji

Jaji mweupe nchini Afrika Kusini amejiuzulu baada ya kutoa matamshi mwaka jana katika mitandao ya kijamii kuwa matukio ya ubakaji ni utamaduni wa watu weusi.

Jaji huyo wa mahama kuu Mabel Jansen alikuwa katika mapumziko akisubiri upelelezi wa mahakama kufanyika juu ya sakata hilo.

Matamshi hayo yalifichuliwa na rafiki yake ambaye hakutajwa jina.

Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi zenye asilimia kubwa ya matukio ya ubakaji duniani.