Trump afanikiwa kubadilisha huduma ya Obamacare bungeni

Rais Trump afanikiwa kubadilisha bima ya afya ya Obamacare katika bunge la uwakilishi
Image caption Rais Trump afanikiwa kubadilisha bima ya afya ya Obamacare katika bunge la uwakilishi

Rais Trump amesema kuwa ana matumaini makubwa kwamba sheria itakayochukua mahala pake huduma ya afya ya Obamacare itapitishwa katika bunge la seneti, baada ya kuidhinishwa na bunge la uwakilishi.

Trump aliyasema hayo wakati alipokuwa akisherehekea ushindi wa kura hiyo.

Wanachama wa Republican wanawapikuwenzao wa Democrat kwa wingi katika bunge la seneti, ikiwemo baadhi ya maseneta amabo wanataka mabadiliko muhimu katika sheria hiyo.

Mwandishi wa BBC mjini washington anasema kuwa muswada huo uliharakishwa ili kuzuia gharama yake ,na idadi ya watu watakaopoteza bima zao za afya haijulikani.