Uzani mkubwa wamkosesha huduma ya kukatwa kucha saloon

Kimberly Adie na mpenzi wake Haki miliki ya picha Kimberly
Image caption Kimberly Adie na mpenzi wake

Mwanamke mmoja nchini Canada anayesema kuwa alinyimwa huduma ya kukatwa nywele katika saloon kutokana na uzani wake mkubwa anasema kuwa alitangaza hadharani kuhusu kisa hicho.

Kimberly Adie mwenye umri wa miaka 27 anasema kuwa wafanyikazi katika Saloon ya Winipig nail walikataa kumuhudumia kutokana na uzani wake mkubwa.

Yeye na mpenziwe walikuwa wamekwenda kukatwa kuchwa wikendi.

Hii sio mara kwanza kwa saloon ya kukata kucha kaskazini mwa Marekani kugonga vichwa vya habari kutokana na vile wanavyowachukulia watu wenye uzani mkubwa.

Saloon kadhaa nchini Marekani pia zimekosolewa kwa kuwatoza ada ya juu wateja wenye uzani mkubwa badala ya kuwalipisha ada ya kawaida.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kimberly Adie asema kwamba alishtuka alipoambiwa kwamba hawezi kuhudumiwa kwa kuwa na uzani mkubwa

Katika kisa hiki cha hivi majuzi ,bi Adie alisema kuwa alipoingia katika saloon hiyo wanawake wawili wanaofanya kazi walimuangalia na mshangao kutoka juu hadi chini.

Baadaye msimamizi wa saloon hiyo alimwambia hawawezi kumuhudumia ,wakidai kwamba hangetoshea.

Mpenziwe aliambia kwamba anaweza kuhudumiwa.

''Nilishtuka sana waliponiambia kwamba singetosha katika viti vyao licha ya kutaka kumuhudumia mpenzi wangu'', alisema.

Bi Adie na mpenzi wake walifululiza hadi katika saloon nyengine .Wakati walipowasili,alisema kwamba alikuwa akibubujikwa na machozi.

''Nilijihisi nina aibu kubwa na nilivyo,lakini mpenziwe alimbembeleza na kuhakikisha kuwa anapata huduma anayotaka''.

Haki miliki ya picha kimberly
Image caption Hatahivyo hatimaye Kimbelry alipata huduma aliokuwa akiihitaji

Amepata ujumbe mwingi tangu alipojitokeza kwa niaba ya wengine wengie ambao wamekuwa wakibaguliwa.