Athari za kupigwa teke kwa Obamacare Marekani

sheria hiyo sasa inapelekwa katika bunge la seneti ambapo itakabiliwa na changamoto kubwa. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption sheria hiyo sasa inapelekwa katika bunge la seneti ambapo itakabiliwa na changamoto kubwa.

Kufuatia kupitishwa kwa sheria mpya ya bima itakayochukua mahala pake sheria ya bima ya afya ya Obamacare na bunge la wawakilishi , sheria hiyo sasa inapelekwa katika bunge la seneti ambapo itakabiliwa na changamoto kubwa.

Iwapo sheria hiyo kama ilivyoandikwa itaidhinisha, itazua hali ya sintofahamu katika mfumo wa afya wa Marekani na kuzilazimu kampuni za bima, watoaji wa huduma za afya na washikadau wa sekta ya afya kukubali mabadiliko mapya miaka michache tu baada ya mabadiliko ya Obamacare kuwakosesha usingizi.

Medicaid ambao ni mpango wa bima ya afya kwa watu masikini utapunguzwa. Mamlaka za bima serikalini zitaondolewa .

Kodi ya watu matajiri waliolipa ruzuku ya bima kwa watu wa mapato ya chini itabatilishwa.

Majimbo yatapewa busara zaidi ili kuondokana na viwango vya chini vya bima.

Kulingana na bajeti ya bunge la uwakilishi ambayo ilichanganua toleo la kwanza la mswada huo, zaidi ya raia milioni 24 wa Marekani hawatakuwa na bima kulingana na sheria ya afya ya Marekani.

Hiyo inamaana kwamba malipo yatashuka kwa zaidi ya asilimia 10.

Mapungufu ya bajeti ya kijimbo yatashuka kwa dola milioni 150 katika kipindi cha miaka 10.

Hathivyo hayo yatabadilika iwapo muswada huo utaidhinishwa wiki ijayo.

Tayari sintofahamu hiyo imeanza kuonyesha madhara yake.

Kampuni ya mwisho iliokuwa ikiwania kuwapatia bima watu binafsi huenda ikajiondoa.

Tayari kampuni nyengine ya bima imeamua kujiondoa katika jimbo la Virginia.

Katika majimbo kadhaa sheria hiyo kwa wale wasio na bima ya afya ya serikali ama hata waajiri wa kibinafsi wanakabiliwa na wasiwasi.

Kwa muda sasa ilionekana kana kwamba bima ya afya ya Obamacare ingeendelea kutoa mwendelezo.

Badala yake mabadiliko makubwa yanaendelea kubisha hodi.

Swala ambapo bunge la seneti huenda likaweka marekebisho yake, litazidisha hali hiyo ya sintofahamu.