Familia moja yaondoshwa kwenye ndege Marekani sababu ya mtoto

Bw Schears na watoto wake wawili waliondoshwa kwa lazima ndegeni Haki miliki ya picha BRIAN SCHEAR
Image caption Bw Schears na watoto wake wawili waliondoshwa kwa lazima ndegeni

Shirika la usafiri wa ndege Marekani, Delta Air Linesis, limekubwa na uhusiano mmbaya kwa umma, baada ya familia moja kudai kuwa waliondolewa ndegeni, kwa kosa la kumnyima mtoto kiti cha kukalia.

"Hili ni kosa la kitaifa na sasa wewe na mke wako mtafungwa jela, na watoto wenu watalindwa na taifa," mfanyikazi mmoja wa ndege alisikika akiiambia familia hiyo.

Video iliyowekwa katika mtandao wa YouTube kuhusiana na kisa hicho, imepata zaidi ya watazamaji milioni mbili.

Kampuni ya Delta inasema kuwa, "samahani kwa tendo hilo la kutamausha" na tutafidia familia hiyo.

Tendo hilo linafuatia kisa cha mwezi uliopita ambao abiria Dkt David Dao, alipo gonga vichwa vya vyombo vya habari, pale alipojeruhiwa alipoondolewa kwa nguvu kutoka ndani ya ndege ya shirika la United Airlines, mwezi uliopita.

Mwezi uliopita, alilipwa kiasi cha pesa ambacho hakijajulikana, baada ya kufikisha kesi mahakamani dhidi ya shirika hilo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Delta Aie Lines

Kisa hicho cha hivi punde, kilifanyika ndani ya ndege iliyokuwa ikitoka Maui huko Hawaii kuelekea Los Angeles mnamo Aprili 23, lakini kikajulikana baada ya mkanda huo wa video kuwekwa mtandaoni.

Video hiyo ya dakika 8 inaonesha Brian Schear, akilalamika kuwa amelipia kiti hicho, ilihali wahudumu wa ndege, akijaribu kumshawishi kuachia kiti hicho, huku Bw Schear akidai kuwa ndege hiyo ilikuwa na abiria wengi kupita kiasi.

Bw Schear, amesema kuwa, awali alikuwa amemlipia kiti mwanawe mkubwa, ambaye alipanda ndege iliyotangulia, kwa hakikisho kuwa mmojawepo wa mwanawe mwingine, atapata kiti ndegeni.

Mmoja wa wahudumu wa ndege awali alimfahamisha kuwa, mvulana wake mwingine alimiliki kiti hicho, kwa hivyo mtoto wake mchanga hataketi pale.

Mwanawe wa miaka miwili, alikuwa ameketi kwenye kiti cha usalama cha watoto, ambacho wahudumu wengine wa ndege walidai kwamba, hatua hiyo imepigwa marufuku chini ya sheria ya kitaifa ya mamlaka ya usafiri wa ndege (FAA) na wakaongeza kuwa mtoto huyo sharti apakatwe.

Mada zinazohusiana