Kenya yazindua kifaa cha kujipimia virusi vya Ukimwi

Upimaji wa virusi vya HIV
Image caption Upimaji wa virusi vya HIV

Kenya imezindua kifaa cha bei nafuu cha kujipimia virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi, ambacho raia wataweza kukitumia bila usaidizi wa daktari.

Kifaa hicho kitaanza kutolewa kwa umma mwezi Julai mwaka huu.

Kifaa hicho kinalenga watu 400,000 ambao hawajafahamu iwapo wana Virusi Vinavyosababisha Ukimwi au la.

Wataalamu wanasema kwamba, kifaa hicho kinafanikiwa asilimia 80, na kitagharimu kama dola 7 hivi na kitapatikana katika maduka ya kuuzia madawa.

Ili kujipima, mtu anatoa mate, damu au majimaji kutoka mwilini na kisha anajipima binafsi bila ya kusaidiwa na mtu.

Martin Sirengo, kiongozi mkuu wa shirika la kukabiliana na Ukimwi Kenya, Nascop, anasema kuwa bado watu watahitajika kwenda hadi katika vituo vya matibabu ili kuthibitisha matokeo.

Haki miliki ya picha TWITER
Image caption NASCOPE

Aidha anashauri kuwa, mtu anafaa kujipimia katika sehemu za faragha na mbele ya mtu anayeaminika.

Rudolf Eggers, mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Kenya, anasema kwamba, "lengo kuu la kifaa hicho cha kujipimia virusi vya HIV ni sambamba na njia nyingine zilizopo za kupima HIV."

Takriban watu milioni 1.5 wanaishi na virusi vya HIV nchini Kenya, ambapo milioni moja kati yao wanatumia matibabu ya kumeza vidonge vya kupunguza makali ya ugonjwa wa Ukimwi.

Mada zinazohusiana