Masaibu ya kuzaliwa na jinsia mbili Kenya

Masaibu ya kuzaliwa na jinsia mbili Kenya

Mamilioni ya watoto wanaozaliwa na jinsia mbili nchini Kenya wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kuishi na jamii inayowazunguka.

Wanakumbana na ubaguzi,unyanyasaji na hata pengine kuuawa.

Mwandishi wa BBC wa masuala ya afya Anne Soy amempata moja ya waliowahi kujificha kukwepa kuuawa kutokana na kuwa na jinsia mbili.