Republicans watilia 'shaka' muswada wa afya wa Trump

Kiongozi wa chama cha Democrats bungeni Nancy Pelosi
Image caption Kiongozi wa chama cha Democrats bungeni Nancy Pelosi

Seneta maarufu katika chama cha Rais Trump cha Republican ameonya kuwa haitakuwa rahisi kwa wabunge kukubaliana juu ya mpango mpya wa kuchukua nafasi ya bima ya afya iliyoanzishwa na Rais Mstaafu Barack Obama ijulikanayo kama Obamacare.

Obamacare ulikuwa mfumo wa bei nafuu wa bima ya afya.

Lakini Seneta mwingine, Orinn Hatch atakayeshiriki katika kutunga sheria mpya ya kufutiliwa mbali mfumo wa bima ya Obamacare alisema licha ya upinzani mkali atahakikisha wabunge wanapitisha hoja hiyo.

Mnamo Alhamizi bunge la wawakilishi lilipitisha kwa uchache wa kura sheria inayokusudia kufutilia mbali mfumo wa bima wa Obamacare.

Image caption Rais wa Marekani Donald Trump

Hata hivyo wanachama wa Republican wana wabunge wachache tu kuwazidi wenzao wa Democratic na kuna baadhi ya hao Warepublican ambao hawaungi mkono kufutiliwa mbali kwa mfumo wa bima ya Obamacare.

Naye Seneta wa chama cha Democratic, Bernie Sanders amesisitiza kuwa muswada huo wa bima wa chama cha Democratic hautapitishwa kwenye bunge la Seneti, akisema mswada huo unapaswa kutupwa chooni wala sio kupitishwa na ye yote.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii