Watu wapiga kura kumchagua rais mpya Ufaransa

Watu wakipiga kura huko Lyon Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Watu wakipiga kura huko Lyon

Watu wa Ufaransa wamekuwa wakijitokeza kupiga kura katika duru ya pili na ya mwisho ya uchaguzi wa rais.

Mashindano leo ni baina ya Emmanuel Macron wa msimamo wa wastani, na Marine Le Pen wa mrengo wa kulia sana.

Vyama vikuu vya siasa, cha kisoshalisti, na cha Republicans cha kati-kulia, vilishindwa katika duru ya kwanza.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mgombea wa urais nchini Ufaransa Emmanuel Macron amedai kwamba wadukuzi waliidukua kampeni yake

Ulinzi ni mkali, baada ya mashambulio ya kigaidi ya hivi karibuni nchini Ufaransa.

Kwa sababu ya kanuni za uchaguzi, wagombea hawana ruhusa ya kuzungumza juu ya udukuzi uliofanywa dhidi ya kampeni ya ya Bwana Macron.

Rais anayeondoka Francois Hollande ameapa kukabiliana vilivyo na wahusika katika udukuzi huo wa kimitandao.

Kamati ya kampeni ya mmoja wa mgombea wa urais nchini Ufaransa, Emmanuel Macron, imesema kuwa imevamiwa vikali na makundi ya udukuzi ambayo yamechapisha habari muhimu ya kundi lao katika mitandao ya kijamii.

Image caption Mpinzani mkuu wa Macron katika uchaguzi wa Urais nchini Ufaransa Marine Le Pen

Washiriki wa Bwana Macron wamesema kuwa barua pepe sahihi zimeibwa katika tarakilishi zao na kuchanganywa na zile bandia ili kuonyesha kuwa kamati hiyo ya Bwana Macron ni ya ubabaishaji tu.

Chama cha Bwana Macron kijulikanacho nchini kama "En Marche" kilisema kuwa wachapishaji wa habari hizo zilizovuruja wana nia ya kuvuruga demokrasia kabla ya uchaguzi wa marudio ya hapo kesho.

Tume ya Uchaguzi nchini Ufaransa inatarajiwa kuongoza mkutano wa dharura baadaye hii leo kujadili madai hayo ya udukuzi.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Ulinzi umedumishwa