Milio ya risasi yasikika katika maeneo salama Syria

Ghasia zimeendelea katika maeneo yaliotengwa kuwa ya salama licha ya mwafaka wa kusitisha vita kuafikiwa Syria Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ghasia zimeendelea katika maeneo yaliotengwa kuwa ya salama licha ya mwafaka wa kusitisha vita kuafikiwa Syria

Raia wa Syria wanasema kuwa milipuko ya makombora na milio ya risasi imesikika katika eneo linalothibitiwa na waasi la Kaskazini Magharibi, muda mfupi baada ya mwafaka wa kubuni maeneo salama kutekelezwa

Mapatano hayo kuhusiana na maeneo salama ambayo yanasema kila upande unapaswa kusitisha mapigano yaliafikiwa mnamo Alhamisi kati ya Urusi na Iran, ambapo wote wanaunga mkono Serikali ya Syria.

Makundi ya waasi yalikataa kushiriki mapatano hayo, ambapo hayakufurahia kushirikishwa kwa Iran.

Inaripotiwa kuwa Uturuki, ambayo inaunga mkono waasi, itahakikisha mkataba huo unatekelezwa, huku Uturuki na Urusi ikisema Marekani, Umoja wa Mataifa na Saudia wote wanaunga mkono mpango huo.

Urusi inasema maeneo yaliyoandaliwa kuwa salama yataenea katika mkoa unaosimamiwa na waasi wa Idlib pamoja na Latakia, Aleppo, Hama, Homms na eneo dogo linalokaliwa na waasi katika mji wa Damascuss.