Kanye West atoweka katika mitandao ya kijamii

Kanye West atoweka katika mitandao ya kijamii Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kanye West atoweka katika mitandao ya kijamii

Msanii wa muziki wa Rap nchini Marekani Kanye West amefuta akaunti zake za Twitter na zile za Instagram ambazo zilikuwa na makumi ya mamilioni ya wafuasi.

Sababu hazijulikani lakini mwezi Novemba mwaka jana alimaliza ziara yake mapema.

Alimshtumu mwanamuziki mwenza Jay Z kwa kujaribu kumuua na kuondoka katika jukwaa baada ya kutangaza kwamba atampigia kura rais wa Marekani Donald Trump wakati wa uchaguzi wa taifa hilo.

Mkewe nyota wa Raality TV Kim Kardashian amesalia katika mtandao wa Twitter na ana wafuasi milioni 51.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Hivi ndivyo ilivyokuwa wakati mashabiki walipojaribu kuwasiliana na msanii huyo

Amekuwa akijikuza pamoja na kampuni ya kuuza nguo ya mumewe.

Muda mfupi baada ya akaunti zake za mitandao kufungwa mkewe alichapisha ujumbe katika mtandao wake wa Twitter kwamba amechora nembo ya kampuni hiyo katika mkono wake.

Mashabiki walimsihi Kardashian amwambie mumewe arudi katika mtandao.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Hivi ndivyo ilivyokuwa katika mtandaoo wa Twitter wa mkewe Kim Kardashian

West alikuwa ameanza kuishi maisha ya ukimya katika mitandao ya kijamii mapema mwaka huu na alidaiwa kufuta ujumbe wake uliokuwa ukimuunga mkono rais Donald Trump.

Hatua yake pia ilijiri baada ya mkewe kuibiwa vito vyenye thamani ya dola milioni 10.5 mjini Paris mwezi Oktoba.