Wakimbizi wampa mtoto wao jina la waziri mkuu wa Canada

Wakimbizi wampa mtoto wao jina la waziri mkuu wa Canada Haki miliki ya picha AFRAA BILAN
Image caption Wakimbizi wampa mtoto wao jina la waziri mkuu wa Canada

Wakati Muhammad na Afraa Bilan waliwasili Canada mwezi Februari mwaka uliopita, walikuwa wanmeanza maisha mapya katika nchi tofauti kabisa.

Wakitokea mjini Damscus nchini Syria, wawili hao pamoja na binti yao Naya na Nael, ambaye ni mtoto wa kiume waliwasili mjini Montreal kama wakimbizi.

Waziri mkuu Justin Trudeau hakuwepo kuwakaribisha kati uwanja wa ndege vile alifanya wakati wakimbizi wengine waliwasili.

Lakini wanandoa hao walihisi kuwa walistahili kumshukuru kwa njia nyingine, na hivyo walimpa mtoto wao aliyezaliwa nchini Canada jina la waziri mkuu Justin Trudeau.

Haki miliki ya picha FACEBOOK/MUHAMMAD BILAN
Image caption Mjini Damascus Muhammad alikuwa akifanya kazi kama kinyozi. Lakini wakati mmoja alishikwa na jeshi la Syria na kufungwa.

Justin Trudeau Adam Bilan alizaliwa siku ya Alhamisi katika mji wa Calgary.

Mjini Damascus Muhammad alikuwa akifanya kazi kama kinyozi. Lakini wakati mmoja alishikwa na jeshi la Syria na kufungwa.

Baada ya kuachiliwa familia yake iligundua kuwa mamlaka zilikuwa zikimtafuta tena na kwamba angefungwa.

Fusra ya kuondoka nchini humo iliwadia wakati waligundua kuwa Canada ilikuwa ikiwachukua wakimbizi wa Syria baada ya bwana Trudeau kuingia ofisini

Miaka mitano ya vita nchini Syria , walifanikiwa kupata fursa hiyo.

Haki miliki ya picha FACEBOOK/MUHAMMAD BILAN
Image caption Justin Trudeau Adam Bilan alizaliwa siku ya Alhamisi katika mji wa Calgary.