Mwanamke atafuna na kumeza $9,000 Colombia

Noti za dola 100 Haki miliki ya picha Getty Images

Mwanamke mmoja nchini Colombia alitafuna na kumeza pesa zote alizokuwa amejiwekea kama akiba, kuzuia mumewe asizichukue na kuzitumia.

Sandra Milena Almeida alimeza £7,000 ($9,000) baada ya kugundua kwamba mumewe alikuwa na mpenzi mwingine.

Hatua yake iligunduliwa baada yake kukimbizwa hospitalini akilalamika kutokana na maumivu makali tumboni.

Madaktari walipata mabunda ya noti katika tumbo lake.

Bi Almeida, 30, yamkini awali alificha pesa hizo baada ya kusikia taarifa kwamba mumewe hakuwa mwaminifu kwake.

Lakini aliamua kuzila noti hizo za $100 baada ya mumewe kugundua eneo alimokuwa ameficha pesa hizo na kudai agawiwe nusu yake.

Jamaa na madaktari waligundua kitendo alichokuwa amefanya mwanamke huyo baada ya kumpima.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Noti zilizotolewa tumboni mwa Sandra

Mkurugenzi wa upasuaji katika hospitali ya chuo kikuu cha Santander, Juan Paulo Serrano, aliambia wanahabari: "Noti 57 za $100 zilipatikana na kutolewa tumboni mwake.

"Nyingine zilipatikana katika utumbo wake mkubwa."

"Yamkini kilikuwa kitendo cha kutamauka, kutokana na tatizo lililomkabili. Hili bila shaka lilimwathiri tumbo."

Mrs Almeida, anayetoka Piedecuesta, anatarajiwa kupata nafuu kabisa baada ya upasuaji huo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bw Serranoa anasema mwanzoni alidhani mwanamke huyo alikuwa mlanguzi wa mihadarati

Bw Serrano alisema baadhi ya noti zilioshwa na zinaweza kutumika tena.

Hata hivyo kunazo ambazo ziliathiriwa na kemikali tumboni.

Bi Almeida amesema sasa ataweka akiba pesa za kwenda likizo ya kifahari.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii