Waliokuwa waasi wafunga barabara Ivory Coast

Rais Ouattara alichukua madaraka baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2010 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Ouattara alichukua madaraka baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2010

Waliokuwa waasi nchini Ivory Coat wanaondamana kwenye mji wa pili kwa ukubwa nchini Ivory Coast, wamefunga barabara inayoelekea katika mji wa kibiashara wa Abidjan na mji mkuu Yamoussoukro.

Wanata kulipwa dola 20,000 kila mmoja pamoja na ajira katika jeshi la serikali kwa mujibu wa Amadou Ouattara, ambaye alijiita kuwa msemaji kwa kundi hilo.

Tunamuomba Rais Alassane Ouattara kuwafikiria wanawe ambao wameteseka kwa miaka 15.

Baadhi ya waasi walikuwa wamejihami na walikuwa wamejipaka majivu usoni.

Waasi kutoka Bouake na maeneo mengine Kaskazini mwa Ivory Coast walimsaidia Rais Ouattara kuchukua madaraka mwaka 2011, baada ya kiongozi wa wakati huo Laurent Gbagbo kukataa kukubali kushindwa.

Image caption Waasi wanata kulipwa dola 20,000 kila mmoja pamoja na ajira katika jeshi