'Spoken word': Sanaa na haki za jamii Kenya
Huwezi kusikiliza tena

'Teardrops': Bingwa wa mashairi ya kisasa Kenya

Kazi za Sanaa huwa zinalenga kuburudisha na kufurahisha hadhira. Hata hivyo sanaa ya mashairi ya kisasa ama 'spoken word' nchini Kenya imeonekana kuchukua mkondo wa kuangazia masuala sugu katika jamii kama vile ufisadi, umaskini na uhalifu.

Anthony Irungu amezungumza na mwana mashairi maarufu 'Teardrops' kuhusu albamu yake mpya 'Made in Eastlands' inayoangazia hali ya maisha katika eneo linaloogopewa na wengi mashariki ya Nairobi, ama 'Eastlando' , pamoja na tasnia ya ushairi nchini Kenya.