Pacha walioshikana Tanzania walio na ndoto kuu

Pacha walioshikana Tanzania walio na ndoto kuu

Ni karibu miongo miwili sasa, tangu mapacha walioungana, Consolata na Maria, walipozaliwa nchini Tanzania.

Mara tu baada ya kuzaliwa, walianza kutunzwa na Kanisa Katoliki, na kujitahidi kuishi maisha ya kawaida, kadri inavyowezekana.

Mwezi huu, wamefikia hatua muhimu sana maishani mwao, kwa kufanya mitihani yao ya mwisho ya sekondari. Mwandishi wetu Leonard Mubali aliwatembelea.