Obama alimuonya Trump kuhusu Flynn

Luteni Jenerali mstaafu Mmmichael Flynn alikuwa ameteuliwa kuwa mshauri wa maswala ya kisiasa wa bwana Trump Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Luteni Jenerali mstaafu Mmmichael Flynn alikuwa ameteuliwa kuwa mshauri wa maswala ya kisiasa wa bwana Trump

Rais Barrack Obama alimuonya rais mpya wa Marekani Donald Trump dhidi ya kumteua Michael Flynn kuwa mshauri wake wa maswala ya usalama wa kitaifa , ikulu ya Whitehouse imethibitisha.

Bwana Obama alimuonya mrithi wake chini ya saa 48 baada ya uchaguzi wa mwezi Novemba wakati wa mazungumzo katika afisi ya rais, waliokuwa maafisa wa Obama wamesema.

Mawasiliano ya bwana Flynn na mjumbe mmoja wa Urusi yalimfanya kuwa rahisi kufanya usaliti jopo la seneti liliarifiwa siku ya Jumatatu.

Alifutwa kazi mnamo mwezi Februari kwa kuficha mawasiliano hayo.

Bwana Flynn ambaye ni luteni jenerali aliyestaafu aliudanganya utawala wa Trump kuhusu kuzungumza vikwazo vya Marekani dhidi ya Urusi na mjumbe wa taifa hilo Sergei Kislyak kabla ya Trump kuidhinishwa kuwa rais.

Katibu wa maswala ya habari Sean Spiecer alisema kwamba ni kweli rais Obama aliweka wazi kwamba hakumpendelea Jenerali Flynn.

Lakini Spicer alisema kuwa hilo sio kujambo la kushangaza kwa kuwa jenerali Flynn alikuwa amefanya kazi na rais Obama na kwamba alikuwa mkosoaji mkubwa wa rais huyo hususan kwa kushindwa kwake kuwa na mipango ya kulikabili kundi la IS na vitisho vyengine vilivyokuwa vikikabili Marekani.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii