Gavana aliyetusi Uislamu afungwa Indonesia

Gavana wa mji mkuu wa Indonesia aliyekufuru kwa kutusi Uislamu Basuki Tjahaja Purnama afungwa Haki miliki ya picha AFP
Image caption Gavana wa mji mkuu wa Indonesia aliyekufuru kwa kutusi Uislamu Basuki Tjahaja Purnama afungwa

Gavana wa jimbo la Jakarta anayeondoka mamlakani amehukumiwa kifungo cha miaka miwili kwa kukufuru na kuchochea ghasia.

Basuki Tjahaja Purnama anayejulikana kama Ahok ,alikuwa mkristo wa kwanza na raia wa Uchina kusimamia mji mkuu wa Indonesia na kesi hiyo ilionekana kuwa kipimo cha uvumilivu miongoni mwa dini tofauti nchini humo.

Alituhumiwa kwa kutusi Uislamu akitaja mstari mmoja katika Koran wakati wa kampeni.

Bwana Purnama alikana kukufuru mahakamani na akasema kuwa atakata rufaa.

Matamshi yake kuhusu Uislamu yalizua hisia kali miongoni mwa viongozi wa dini hiyo walio na msimamo mkali.

Walifanya maandamano ya mara kwa mara wakitaka ashitakiwe huku baadhi ya Waislamu wenye msimamo mkali wakitaka anyongwe.

Kabla ya hukumu hiyo kutolewa waandamanaji waliomuunga mkono na wale waliokuwa wakimpinga walitaka aachiliwe huru huku wengine wakitaka afungwe jela kwa muda mrefu.

Takriban maafisa 15,000 wa usalama kutoka maafisa wa polisi na jeshi wanaweka usalama katika eneo hilo huku maafisa wa polisi wa kukabiliana na ghasia na magari ya kivita yakiyatawanya makundi hayo mawili.

Mada zinazohusiana