Mwanamke mzito duniani augua ugonjwa wa moyo

Eman Abd El Aty wakati alipokuwa akisafirishwa kutoka India hadi Abu Dhabi kwa matibabu zaidi Haki miliki ya picha Empics
Image caption Eman Abd El Aty wakati alipokuwa akisafirishwa kutoka India hadi Abu Dhabi kwa matibabu zaidi

Mwanamke wa Misri aliyeaminika kuwa mtu mzito zaidi duniani sasa anatibiwa matatizo kadhaa ya kiafya katika hospitali moja ya Abu Dhabi.

Eman Abd El Aty aliyedaiwa kuwa na uzani wa kilo 500 aliondoka katika hospitali moja ya India wiki iliopita baada ya madaktari kusema kuwa alipoteza zaidi ya takriban kilo 250.

Lakini madaktari huko UAE sasa wanasema anaugua magonjwa ya moyo pamoja na vidonda vilivyosababishwa na kulalalia kitanda kwa muda mrefu mbali na uzito wake wa kupita kiasi.

Katika majuma ya hivi majuzi ugomvi ulizuka kati ya madaktari nchini Idnia na familia yake.

Ulianza baada ya dadaake ,Shaimaa Selim kutoa kanda fupi ya video katika mitandao ya kijamii akidai kwamba dadaake alikuwa hawezi kuzungumza na hata kutembea kinyume na ilivyodaiwa na hospitali hiyo.

Hospitali hiyo ilikana madai hayo.

Image caption Madaktari wa Abu Dhabi sasa wanasema kuwa bi Eman Abd anaugua magonjwa tofauti

Taarifa iliotolewa na Hospitali ya Burjeel huko Abu Dhabi imesema kuwa kundi la madaktari 20 linamtibu bi Abd El Aty.

Kwa sasa anakabiliwa na magonjwa kadhaa ya kiafya, ikiwemo tatizo la moyo ambalo bado linachunguzwa, maambukizi ya njia ya mkojo pamoja na vidonda vinavyosababishwa na kulalia kitanda kwa muda mrefu.

Mada zinazohusiana