Raia wa Korea Kusini kumchagua rais mpya

Raia wa Korea Kusini wanapiga kura ili kumchagua rais mpya kufuatia kashfa iliomkabili rais aliyetimuliwa mamlakani Park Geun Hye Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Raia wa Korea Kusini wanapiga kura ili kumchagua rais mpya kufuatia kashfa iliomkabili rais aliyetimuliwa mamlakani Park Geun Hye

Raia wa Korea Kusini hii leo wanapiga kura kumchagua Rais mpya kuchukua nafasi ya Park Geun-Hye, aliyepatikana na makosa na kushtakiwa kwa madai ya ulaghai.

Mgombea Urais kutoka chama cha Liberal, Moon Jae-in ametaja kuwa angependa kuimarisha uhusiano na Korea Kaskazini.

Vyombo vya habari Korea Kaskazini vimesema kuwa vingependelea uongozi uliokuwa wa zamani ambapo mataifa hayo mawili yalikuwa ya kishirikiana na kuwasiliana.

Mgombea anayeegemea mrengo wa kushoto yuko kifua mbele huku yele mwenye msimamo wa kadri Ahn Cheol-soo akiwa mpinzani wake mkubwa.

Uchaguzi huo unaangaliwa wakati ambapo kuna tataizo la kiuchumi nchini humo na wasiwasi na Korea Kaskazini.

Bwana Moon anataka kuimarisha mawasiliano na Korea Kaskazini kinyume na aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo Park Geun Hye ambaye alikata uhusiano wote na taifa hilo.

Wachunguzi wanatarajia idadi kubwa ya watu kujitokeza huku idadi hiyo ikipigwa jeki na wapiga kura vijana huku Korea Kusini ikichagua rais kutoka kwa wagombea 13.

Mada zinazohusiana