Uchafu wa soko wampa ajira mwanamke Tanzania

Wanawake barani Afrika wameendelea kujitosa katika kazi mbalimbali ili kujikomboa kiuchumi.

Huko nchini Tanzania mwanamke mmoja jijini Dar es salaam anafanya kazi ya kuosha watu miguu nje ya soko la Mabibo mara tu watokaponunua bidhaa mbalimbali katika soko hilo.

Sarafina anasema kuwa uchafu wa sokoni hapo ndio ulimpa wazo la kuanzisha biashara hiyo.

Mwandishi wetu Munira Hussein alifika sokoni hapo na kutuandalia taarifa ifuatayo.