Waliokabiliana na ufisadi FIFA waachishwa kazi

Cornel Borbely na Hans-Joachim Eckert walikuwa wamemaliza kipindi chao cha miaka minne Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Cornel Borbely na Hans-Joachim Eckert walikuwa wamemaliza kipindi chao cha miaka minne

Uongozi wa shirikisho la soka duniani FIFA umeamua kuwaachisha kazi mchunguzi mkuu wa maswala ya maadili na jaji wake ambao walihusika pakubwa katika kukabiliana na ufisadi.

Maafisa hao Cornel Borbel y na Hans-Joachim Eckert walisaidia kumuondoa madarakani aliyekuwa rais wa shirikisho hilo wa muda mrefu Sepp Blatter na mkuu wa shirikisho la soka barani Ulaya Michel Platini.

Wawili hao wamepinga hatua hiyoambayo wanasema kuwa iinasitisha mpango wa mabadiliko katika shirikisho hilo.

Waliwashtumu maafisa wa ngazi za juu katika shirikisho hilo kwa kuweka mbele maslahi yao ya kisiasa badala yale ya siku za usoni ya shirikisho hilo.

Uamuzi huo wa baraza kuu la Fifa ulitangazwa nchini Bahrain siku ya Jumanne siku mbili kabla ya kufanyika mkutano wa 67 wa shirikisho hilo.

Mada zinazohusiana