Moon ala kiapo kuongoza Korea kusini

Rais mpya wa Korea kusini akiwa na mkewe Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais mpya wa Korea kusini akiwa na mkewe

Rais mpya wa Korea kusini Moon Jae-in amekula kiapo cha kuiongoza nchi hiyo kufuatia ushindi alioupata katika uchaguzi wa jana Jumanne.

Bwana Moon ambaye ni wakili na mtetezi wa haki za binadamu aliye ahidi kuimarisha uhusiano mzuri na Pyongyang, amesema atafanya kazi ili kudumisha amani.

Amesema anajiandaa kuitembelea Marekani, China na hata Pyongyang iwapo hali itakuwa sawa.

Leo pia anatarajiwa kuitangaza timu yake ya uongozi serikalini.