Ongezeko la vifo vya watoto Venezuela

Wanawake wa Venezuela Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanawake wa Venezuela

Kumetokea ongezeko kubwa la watoto na akina mama wanaofariki nchini Venezuela.

Wizara ya Afya imesema kuwa idadi ya wanawake wanaofariki wakati wa kujifungua imeongezeka kwa asilimia 65 na idadi ya watoto wanaofariki wanapozaliwa imefikia asilimia 30.

Kumekuwa na ongezeko pia la magoinjwa kama vile malaria na Donda koo.

Venezuela imekuwa ikikabiliwa na uhaba mkubwa wa takriban dawa zote