Ndovu wavamia chuo kikuu cha Dodoma Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Ndovu wavamia chuo kikuu cha Dodoma Tanzania

Mara nyingi tumezoea kusikia Tembo wamevamia kijiji au mashamba na kufanya Uharibifu. Jana pia katika Chuo Kikuu cha Dodoma katikati mwa Tanzania walipata ugeni wa tembo wanne wakiwa karibu kabisa na mabweni wanayolala wanafunzi. Lakini ni kweli kuwa mara zote tembo ndio wavamizi?

Kujua hilo, awali nimezungumza na Paschal Shelutete Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA kutaka kujua pia hali ilivyokuwa baada ya tembo hao kuonekana katika eneo hilo.