Lula Da Silva apandishwa kizimbani

Lula Da Silva Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Lula Da Silva

Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva ametoa ushahidi mbele ya Jaji wa nchi hiyo anayeshughulika na masuala ya kupambana na rushwa katika kesi yake ya kwanza kati ya tano zinazomkabili.

Ni sauti ya Jaji wa ngazi ya juu anayehusika na masuala ya rushwa Sergio Moro katika lugha ya kihispania, akimjulisha mtuhumiwa Rais wa zamani kwamba atatendewa haki katika kesi hiyo, na pia kutokana na kazi yakev aliyoifanya kipindi cha nyuma na kusisitiza kumkakikisdhia hilo.

Na baada ya hapo alimhoji kiongozi huyo wa zamani kwa takriban saa tano.

Katika hotuba yake iliyojaa hisia kwa maelfu ya washabiki wake nje ya mahakama hiyo Lula da Silva alisema watu wanaomshtaki hawakupata ushahidi wowote dhidi ya mashtaka makuu yanayomkabali kwamba alipokea nyumba kama hongo katika kashfa ya rushwa inayohusisha kampuni ya mafuta ya taifa ya nchi hiyo, Petrobras.

Amesema suala hilo halitamzuia juhudi zake za kugombea nafasi ya irais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2018.

Akizungumza muda mfupi baada ya kesi hiyo kusikilizwa mmoja ya mawakili wake Valeska Zanin amesema kesi hiyio inamsukumo wa kisiasa.

Kwa upande wake wakili mwingine wa Bwana Lula da Silva Cristiano Marttins amesema mteja wake hana hatia na kuongeza kuwa shutuma za mteja wake kwamba alipokea makazi hayo kama hongo si za kweli.

Iwapo Rais huyo mstaafu atakutwa na hatia, atahukumiwa kifungo gerezani.