Maandamano yasababisha vifo Venezuela

Waandamanaji Venezuela Haki miliki ya picha ALEJANDRO CEGARRA
Image caption Waandamanaji Venezuela

Watu wengine wawili wameuawa katika siku nyingine ya maandamano ya kupinga Serikali nchini Venezuela, ambapo watu waliofariki kwa mwezi uliopita kufika 40.

Waandamanaji wachanga katika mji wa Caracas waliwatupia wanajeshi chupa na kinyesi cha wanadamu huku maafisa wa usalama wakiwapuliza na gesi ya kutoa machozi na kuwamwagia maji kutoka magari makubwa maalumu ya kuzima ghasia.

Wakati maandamano hayo yakienmdelea, wanaounga mkono serikali nao pia walifanya yao, wakicheza Salsa na kuonesha picha ya aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Hugo Chavez.