Dawa za Wanajihad zanaswa Uholanzi

Dawa za Wanajihad zanaswa Uholanzi Haki miliki ya picha DUTCH POLICE
Image caption Dawa za Wanajihad zanaswa Uholanzi

Maafisa wa polisi wa Uholanzi wanawatafuta washukiwa wawili baada ya maabara ya dawa kupatikana na furushi moja la dawa zinazopendwa sana na wanajihadi.

Maafisa hao walikuwa wamebaini walikuwa wamegundua dawa bandia za Capton na kusema hawajui iwapo zilikuwa zikipelekwa mashariki ya kati.

Wakati huohuo maafisa wa maswala ya fedha walifichua wiki hii wamefanikiwa kunasa dawa milioni 37.5 aina ya Tramadol ambazo hutumiwa na wapiganaji wa IS.

Mzigo huo ulikuwa unaelekea Libya.

Haki miliki ya picha GUARDIA DI FINANZA
Image caption Dawa aina ya Tramadol hutumiwa sawa na wapiganaji wa Boko haram nchini Nigeria

Maafisa wa polisi wa Itali wanasema kuwa mzigo huo ulikuwa umetoka India na ungetumika kwa sababu mbili: Kusaidia kufadhili ugaidi na matumizi kwa wanajihad ili kujisisimua na kukabiliana na shinikizo la kiakili.

Utumizi wa Tramadol ulielezewa na ripoti kuwa wa kiwango cha juu miongoni mwa wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria na huenda ilitumika katika kusababisha mauaji katika pande zote mbili za mzozo.

Mada zinazohusiana