Hisa za Snapchat zashuka

Mtandao wa Snapchat Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mtandao wa Snapchat

Hisa za mtandao wa Snapchat zimeshuka baada ya ripoti ya ukuaji mdogo katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza mwaka huu.

Katika matokeo yake ya kwanza tangu hisa hizo ziwekwe katika soko la hisa ,snachat imesema kuwa wateja wake wa kila siku waliongezeka asilimia 5 pekee na kufikia milioni 166 ikilinganishwa na kipindi cha miezi mitatu ya mwisho 2016.

Idadi hiyo ni milioni 2 chini ya ilivyotarajiwa, lakini ni ya juu kwa asimilia 36 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita.

Habari hizo zilisababisha hisa kushuka kwa asilimia 20 baada ya biashara mjini New York.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ripoti ya Snapchat

Wawekezaji hawakutarajia mapato ya juu na walihisi kukatika tamaa.

Hasara kubwa, ukuwaji mbaya na ishara hafifu kwamba mtandao huo hauna chochte cha kuvutia ili kukabiliana na ushindani wa mtandao facebook.

Mkurugenzi mkuu wa Snapchat Evan Spiegel alisema kuwa wateja wake wachache wa kila siku sio wasumbufu.

Mada zinazohusiana