Familia yaasili watoto saba ndugu Marekani

Clark Haki miliki ya picha Jessaka Clark/Facebook

Mume na mke nchini Marekani wamechukua hatua isiyo ya kawaida, ya kuwaasili watoto saba ambao ni ndugu.

Maria, Elizabet, Guillermo, Jason, Kristina, Katerin na James wamesailiwa na Josh na Jessaka Clark katika jimbo la Georgia.

Watoto hao walikuwa wamekaa katika kituo cha kuwatunza watoto kwa miaka minne.

Walikuwa wamekaa katika kituo hicho kwa siku 1,359 kabla ya ombi la wawili hao kuwaasili kukamilishwa tarehe 9 Mei 2017.

Josh na Jessaka walianza utaratibu wa kuwaasili watoto hao miaka miwili iliyopita.

Watoto hao wamekuwa wakiishi na wawili hao kwa miezi 10 iliyopita.

Josh na mkewe wana mwana mmoja wa kiume wao halisi ambaye jina lake ni Noah.

Jessaka amepakia kwenye Facebook picha ya familia yake kubwa sasa, na amekuwa akiwapasha watu kuhusu yanayojiri katika familia hiyo.

Haki miliki ya picha Jessaka Clark / Facebook
Image caption Jessaka aliweka picha hii kwenye Facebook walipokamilisha utaratibu wa kuwaasili watoto hao

"My husband Josh and I both knew that we wanted to adopt children. We had decided this before we even met each other,"

Jessaka ameambia Fox News kwamba yeye na Josh walijua kwamba wangewaasili watoto hata kabla yao kukutana na kuoana.

"Josh huhurumia sana maelfu ya watoto wasio na wazazi na alitaka kuleta kadha nyumbani kwetu," anasema.

Familia hiyo huenda ikaongezeka kwani wawili hao wamefanikiwa kuchangisha $20,000 (£15,500) kwa kutumia mtandao wa Go Fund Me katika chini ya saa 24.

Wanataka kupanua nyumba yao ili kupata nafasi ya kutosha kwa watoto hao.

Aidha, wamesema wanapanga kuwaasili watoto wengine.

Haki miliki ya picha Jessaka Clark / Facebook
Image caption Jessaka aliandika kwamba alikuwa anaelekea shuleni kubadilisha majina ya watoto hao

Mada zinazohusiana