Trump: Sichunguzwi na FBI

Rais Trump anasema kuwa hachunguzwi Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Trump anasema kuwa hachunguzwi

Rais wa Marekani Donald Trump amesisitiza kwamba hafanyiwi uchunguzi wowote baada ya kumfuta kazi mkurugenzi wa shirika la ujasusi la FBI.

Bwana Trump aliambia chombo cha habari cha NBC kwamba ilikuwa uamuzi wake pekee kumsimamisha kazi James Comey.

Bwana Comey alikuwa akiongoza uchunguzi kuhusu madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani uliokamilika mbali na uwezekano kwamba kulikuwa na mawasiliano kati ya, maafisa wa Trump na Urusi wakati wa kampeni.

Bwana Trump ameutaja uchunguzi huo kuwa unafiki mkubwa madai yaliopingwa na Mrithi wa Comey.

Katika mahojiano yake ya kwanza tangu alipomfuta kazi mkurugenzi huyo , Bwana Trump aliambia NBC siku ya Alhamisi kwamba alimuuliza bwana Comey iwapo alikuwa akimchunguza.

Nilimwambia iwapo inawezekana unaweza kuniambia, Je Ninachunguzwa? Aliniambia ,huchunguzwi.

''Najua sichunguzwi'', Bwana Trump alimwamabia aliyekuwa akimhoji, akirejelea madai aliyotoa katika baraua ya Jumanne ya kumfuta kazi bwana Comey.

Rais huyo pia alipinga maelelezo ya ikuu ya Whitehouse kwamba alimfuta bwana Comey baada mapendekezo kutoka maafisa wakuu wa wizara ya haki.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii