Hoteli yafungwa kwa madai ya kuuza nyama ya ng'ombe India

Ng'ombe nchini India ni wanayama watakatifu na kuna sheria dhidi ya ulaji na uchinjai wa mnyama huyo.
Image caption Ng'ombe nchini India ni wanayama watakatifu na kuna sheria dhidi ya ulaji na uchinjai wa mnyama huyo.

Mmiliki mmoja wa hoteli katika jimbo la Rajasthan nchini India ameonyesha masikitiko yake baada ya hoteli yake kufungwa kwa madai ya uwongo kwamba aliuza nyama ya ng'ombe.

Maafisa wa Polisi siku ya Jumanne walisema kuwa vipimo walivyochukua katika nyama iliopatikana katika hoteli hiyo ya Hayat Rabbani mnamo mwezi Machi vilionyesha kwamba sio nyama ya ng'ombe, bali kuku kulingana na gazeti la Hindustan Times.

Ng'ombe ni wanyama watakatifu miongoni mwa jamii ya Hindu nchini India na kuna sheria kali dhidi ya uchinjaji na ulaji wa wanyama hao katika maeneo mbalimbali ya taifa hilo ikiwemo Rajasthan.

''Kuanzia siku ya kwanza ,nimekuwa nikisema kuwa ni kuku lakini hakuna mtu mmoja aliyenisikiza'', alisema Naeem Rabbani.

''Ripoti hiyo pia ilithibitisha madai dhidi yetu ni ya uwongo''.

Hoteli hiyo ilifungwa baada ya kundi moja la kulinda ng'ombe kufanya maandamano mbele ya hoteli hiyo kwa saa kadhaa mnamo mwezi Machi, wakiimba nyimbo za kitaifa.

Mada zinazohusiana